Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI-HAKI-USHIRIKIANO

Baraza la Haki za binadamu lajiandaa kutafuta mrithi wa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ameonya katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, akitangaza kujitoa kwa Marekanikatika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ameonya katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, akitangaza kujitoa kwa Marekanikatika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Washington. Reuters

Nchi mbalimbali ulimwenguni zimeendelea na mshangao kuhusu uamuzi wa   Marekani wa kujitoa kwenye Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa  siku ya Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na uamuzi huo wa Marekani, uliotangazwa na balozi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley , Rais wa Baraza la haki za binadamu huko Geneva Uswisi, Vojislav Šuc, amethibitisha kwamba uchaguzi wa kumtafuta mjumbe wa kujaza nafasi ya Marekani utafanyika haraka iwezekanavyo.

Wanachama katika Baraza la haki za binadamu huchaguliwa kwa kura nyingi katika Baraza kuu la Umoja wa Mataifa huko New York. Hivyo nitawasiliana na Rais wa Baraza Kuu, Miroslav Lajčák, kuhusu mchakato wa uchaguzi”

Hata hivyo ameongeza kuwa uchaguzi huu utafanyika endapo Marekani itawasilisha rasmi kwa maandishi, taarifa za kujtoa kwenye baraza hilo.

Ofisi ya Bw. Lajčák ilitoa tamko kuhusu kujitoa kwa Marekani ikisema
Marekani ilikuwa na"jukumu kubwa la uhamasishaji wa haki za binadamu"duniani kote, hivyo kujitoa kwao ni pengo kubwa na ni jambo lakusikitisha.

Naye kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein amesema tukio hilo si tu la kushangaza bali ni la kukatisha tamaa kabisa, akiongeza kuwa Marekani inapaswa "kupiga hatua mbele kuliko  kurudi nyuma" kutokana na hali ya haki za binadamu katika dunia ya sasa.

Bwana Zeid amerejelea kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, kwamba "angependelea sana" Marekani kuendelea kubaki katika baraza la haki za binadamu.

Marekani ilitangaza kujitoa katika Baraza la haki za binadamu, kufuatia tuhuma za kuwepo na chuki dhidi ya Israel katika maamuzi mbambali huku ikitaka mabadiliko ya baraza hilo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.