Pata taarifa kuu
MAREKANI-WAHAMIAJI-USALAMA

Mahakama Kuu yaidhinisha marufuku ya Trump kuhusu wahamiaji

Maandamano mbele ya Mahakama Kuu baada ya uamuzi wa kuidhinisha uhalali wa amri ya rais Donald Trump ambayo inapiga marufuku raia kutoka nchi sita zenye Waislam wengi kuingia Marekani,Washington, Juni 26, 2018.
Maandamano mbele ya Mahakama Kuu baada ya uamuzi wa kuidhinisha uhalali wa amri ya rais Donald Trump ambayo inapiga marufuku raia kutoka nchi sita zenye Waislam wengi kuingia Marekani,Washington, Juni 26, 2018. Mark Wilson/Getty Images/AFP

Mahakama Kuu nchini Marekani imeidhinisha marufuku ya Donald Trump inayozuia raia kutoka nchi sita zenye Waislam wengi kuingia nchini Marekani. Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu ya Marekani unahitimisha mvutano wa muda mrefu kati ya majaji.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu ya imeidhinisha marufuku hiyo kwa kura tano dhidi ya nne. Marufuku hiyo iliyozua utata ndani na nje ya Marekani hatimaye imeidhinishwa. Agizo la Trump linaloweka marufuku kwa raia wa nchi sita zenye Waislam wengi ilipitishwa mnamo Januari 27, 2017, wiki moja baada ya rais Trump kuchukua madaraka. Agizo hilo linapiga marufu raia kutoka nchi hizo sita kuingia nchini Marekani. Nchi hizo ni pamoja na Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen na Korea Kusini. Chad pia ilijumuishwa miongoni mwa nchi hizo kabla ya kuondolewa tarehe 10 Aprili mwaka huu.

Lakini kesi haikuhusisha marufuku dhidi ya Korea kaskazini.

Mahakama za chini zilitaja marufuku hiyo kwenda kinyume na katiba, lakini mahakama hiyo ya juu zaidi imepindua uamuzi huu kwa ridhaa ya baadhi ya majaji katika tangazo lililotolewa Jumanne wiki hii.

Uamuzi wa leo wa mahakama ya juu zaidi pia unaidhinisha kuwa rais ana haki ya kuidhinisha marufuku ya aina hii - na wenye maoni ya kulipinga hili hawawezi kuzuia uwezo huu.

Kwa mujibu wa amri hiyo ya Trump, wakimbizi wote wanaofika mipakani mwa Marekani kwa sababu ya kutoroka vita makwao au sababu yoyote nyengine hawataruhisiwa kuingia nchini na mfumo wa upekuzi na ukaguzi wa kina anaouita "extreme vetting" utaidhinishwa.

Rais Donald Trump anasema mikakati hiyo inalenga kuzuia Waislamu walio na itikadi kali kutoingia kabisa Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.