Pata taarifa kuu
MEXICO-USALAMA

Mexico: Milipuko yaua watu 24 katika ghala za fataki

Milipuko yaua watu zaidi ya 20huko Tultepec, Mexico.
Milipuko yaua watu zaidi ya 20huko Tultepec, Mexico. REUTERS

Watu 24 wameuawa katika milipuko miwili katika ghala za fataki huko Tultepec, kilomita 30 kaskazini mwa Mexico. Watu wengi wamejeruhiwa katika tukio hilo, mamlaka imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mlipuko wa kwanza wakati ambapo maafisa wa Ziima Moto, polisi na maafisa wa kikosi cha uokoji walipokua wakiwasili katika eneo la tukio, mlipuko wa pili ulitokea na kusababisha vifo vingi kati ya maafisa hawa, imesema taarifa kutoka mamlaka ya Jimbo la Mexico.

Picha zilizorushwa kwenye televisheni zinaonyesha moshi mkubwa ukifumba juu ya majengo nje kidogo ya mji wa Tultepec, huku maafisa kadhaa wa Zima Moto na waokoaji wakiwa kwenye eneo la tukio.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasema watu 17 wameuawa kwenye eneo la tukio na saba walifarikia wakiwa hospitali. Watu ishirini wamejeruhiwa.

Katika siku za nyuma, milipuko kadhaa ilitokea katika ghala za fataki katika mji wa Tultepec, ikiwa ni pamoja na ile iliyotokea kwenye soko mnamo mwezi Desemba 2016 na kuua watu 30.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.