Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Rais wa Urusi aalikwa kuzuru Marekani

Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, Julai 16,  2018 huko Helsinki.
Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, Julai 16, 2018 huko Helsinki. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump amemwalika rais wa Urusi Vladimir Putin kuzuru nchi hiyo, baada ya kipindi cha joto. Msemaji wa rais wa Marekani Donald Trump amethitisha kuwa rais Trump amepanga kumwalika Rais wa Urusi Vladmir Putin kutembelea Washington, baadaye mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu ya Washingto Donald Trump Sarah Sanders ameiandika Taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter, wakati huu kukiwa na ukosoaji mkubwa kuhusu mkutano wa viopngozi hao wawili uliofanyika siku ya Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland, Helsinki.

Sanders amesema majadiliano kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza na kila kitu kimeandaliwa kufanikisha ziara hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wameipokea taarifa hiyo shingo upande, miongoni mwao ni mwanasiasa anayeongoza maseneta wa chama cha Democrat nchini humo, Chuck Schumer, ambaye amepinga mualiko huo.

Wanasiasa hao wamesema rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana na rais Putin kabla ya kutoa ufafanuzi kuhusu nini kilitokea katika mkutano wake na Putin huko Helsinki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.