Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-HAKI

Venezuela yatakiwa kuanzisha uchunguzi baada ya kifo cha mwanasiasa wa upinzani

Watu wengi wameshtushwa na kifo cha Fernando Alban na kuja moja kwa moja mbele ya makao makuu ya idara ya upelelezi Caracas, Oktoba 8, 2018.
Watu wengi wameshtushwa na kifo cha Fernando Alban na kuja moja kwa moja mbele ya makao makuu ya idara ya upelelezi Caracas, Oktoba 8, 2018. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wametoa wito wa kuanzishwa kwa uchunguzi kuhusu mazingira ya kifo cha mmwanasiasa wa upinzani nchini Venezuela Fernando Alban.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa serikali ya Venezuela "Fernando Alban amejiua", lakini upinzani unasema mwanasiasa huyo aliuawa na serikali.

Fernando Alban, aliyekuwa kizuizini kwa kesi ya madai ya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Rais Nicolas Maduro, amejiua Jumatatu wiki hii kwenye makao makuu ya idara ya upelelezi, amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Tarek William Saab, ambaye ametangaza kwamba "uchunguzi wa kina" umeanzishwa.

Chama cha Fernando Alban, Primero Justicia (Sheria kwanza), kimebaini kwamba mwanasiasa huyo aliuawa na serikali, kikibaini kwenye taarifa: " Maduro na utawala wake wa kimabavu wanahusika na kifo cha Ferdinando Alban".

Kutokana na "habari zinazokinzana na yale yaliyotokea," Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa mataifa imeomba "uchunguzi wa uwazi ufanyike ili kujua mazingira ya kifo chake."

"Fernando Alban amekuwa akizuiliwa na serikali na serikali ilikuwa na wajibu wa kuhakikisha usalama na wake," msemaji wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Ravina Shamdasani, amewaambia waandishi wa habari huko Geneva.

Umoja wa Ulaya pia umetoa wito wa kuanzishwa kwa "uchunguzi wa kina na huru ili kujua mazingira ya kifo cha kutisha cha Ferdinando Alban ," amesema Maja Kocijancic, msemaji wa Mkuu wa sera za mambo ya Nje wa Umoja wa ualaya Federica Mogherini, akikumbusha kwamba " ni wajibu wa serikali kuhakikisha usalama wa watu wote wanaozuiliwa jela. "

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.