Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAUDI ARABIA-MWANAHABARI

Trump: Inaonekana Jamal Khashoogi ameuawa

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumzia hatima ya Mwanahabari Jamal Khashoogi Oktoba 18 2018
Rais wa Marekani Donald Trump akizungumzia hatima ya Mwanahabari Jamal Khashoogi Oktoba 18 2018 Nicholas Kamm / AFP

Rais wa Marekani  Donald Trump amesema inavyooneka, Mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoogi aliyetoweka akiwa ndani ya Ubalozi wa nchi yake, nchini Uturuki, ameuawa.

Matangazo ya kibiashara

Trump amesema inasikitisha sana lakini anasubiri ripoti kamili kabla ya kutangaza hatua ambazo amesema zitakuwa kali kwa uongozi wa Saudi Arabia.

"Nafikiri ameuawa, inasikitisha sana, lakini tunasubiri matokeo ya uchunguzi, kufahamu kilichotokea," alisema Trump.

Khashoogi alionekana akiingia kwenye ubalozi wa nchi yake jijini Instanbul, lakini hakuonekana tena.

Saudi Arabia imekanusha kuhusika na madai ya kuuawa kwa Mwanahabari huyo ambaye amekuwa akiandika makala za kuukosoa uongozi wa Riyadh.

Marekani inasema itaichukulia hatua kali Saudi Arabia iwapo itabainika kuwa ilihusika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.