Pata taarifa kuu
MAREKANI-KIFO-BUSH

Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush afariki dunia

Rais wa zamani wa Marekani George H. W Bush siku akiwa hai
Rais wa zamani wa Marekani George H. W Bush siku akiwa hai Reuters

Rais wa zamani wa Marekani George Herbet Walker Bush, amefariki dunia.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limetolewa na mtoto wake George W.  Bush,  ambaye pia alikuwa rais wa 43 Marekani.

George H. W Bush, alikuwa rais wa 41 wa Marekani na alikuwa madarakani kati ya mwaka 1989 na 1993.

Kati ya mwaka 1989-1993, alihudumu kama Makamu wa rais wakati wa uongozi wa rais Ronald Reagan.

Hadi kifo chake, Bush amekuwa akiugua kwa muda mrefu. Mwezi Aprili, alilazwa hopsitalini baada ya kupata maambukizi katika damu, lakini baadaye akaruhusiwa kuondoka hospitalini.

Amefariki dunia, miezi saba, baada ya kifo cha mkewe Barbara.

“Jeb, Neil, Marvin, Doro na Mimi, tunasikitika kutangaza kuwa baada ya miaka 94, baba yetu amefariki,” ilisomeka taarifa ya George Bush Jr, aliyehudumu rais wa 43 wa Marekani.

“ Alikuwa mtu, mwenye haiba ya juu na baba mwema sana kwa mtoto yeyote wa kiume au kike, angetamani awe naye,” taarifa iliendelea kueleza.

George HW Bush alikuwa nani ?

Alihudumu kwa muhula mmoja, kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993.

Bush atakumbukwa sana kwa mchango wake wa kumaliza vita baridi, na kuimarisha sera ya diplomasia ya Marekani.

Licha ya kuwa na umaarufu wa asilimia 90, mwanasiasa huyo wa chama cha Republican alishtumiwa na wapinzani wake kwa kushindwa kushughulikia mambo ya ndani  hasa uchumi, na wakati wa Uchaguzi wa mwaka 1992, Bill Clinton alimshinda na kumwondoa madarakani.

Alianza kujihusiha na masuala ya siasa na mwaka 1964, baada ya kuanza kujihusisha na biashara ya mafuta, na kufikia umri wa miaka 40, alikuwa Milionea.

Aidha, alikuwa rubani wa ndege za kivita jeshi la Marekani na mwezi Septemba mwaka 1944 aliangushwa na wanajeshi wa Japan, wakati wa vita vya pili vya dunia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.