Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-USALAMA

Donald Trump atishia kutangaza hali ya hatari kwenye mpaka wa nchi yake na Mexico

Donald Trump akitembelea mpaka wa nchi yake na wa Mexico, Texas, Januari 10, 2019.
Donald Trump akitembelea mpaka wa nchi yake na wa Mexico, Texas, Januari 10, 2019. REUTERS/Leah Millis

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kutangaza hali ya hatari kwenye mpaka wa nchi yake na Mexico iwapo, wabunge hawatakubali kumpa fedha za kuanza kujenga ukuta.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa chama cha Democratic wamekataa kupitisha bajeti ya serikali ambayo ingewezesha ujenzi wa ukuta huo, suala ambalo wanasiasa wa Democratic hawataki.

Mvutano huu umeendelea kusababisha kukwama kwa shughuli za serikali, na baadhi ya wafanyakazi kutolipwa mshahara.

Akitembelea mpaka huo, rais Trump amesema ni lazima ukuta huo ujengwe ili kuzuia uingizwaji wa madawa ya kulevya na wahalifu nchini Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.