Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-UCHUNGUZI

Ripoti ya Mueller: Hakuna ushahidi wa makubaliano kati ya Trump na Moscow

Donald Trump azungumza kabla ya kuzuru Palm Beach Machi 24, 2019.
Donald Trump azungumza kabla ya kuzuru Palm Beach Machi 24, 2019. REUTERS/Kevin Lamarque

Waziri wa Sheria wa Marekani Bill Barr amewasilisha kwenye bunge la Congress muhtasari wa ripoti ya Mwanasheria Maalum Robert Mueller kuhusu uchunguzi wa madai ya ushirikiano kati Urusi na timu ya kampeni ya Donald Trump mnamo mwaka 2016.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa ikulu ya White House , kesi hiyo imeweka wazi kuwa rais Donald Trump "amesafishwa" na "hakuhusika na njama na Urusi."

Huu ni ushindi mkubwa kwa Donald Trump. Ripoti ya Mwanasheria Maalum anayehusika na uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imebaini kwamba hakuna njama yoyote kati ya timu ya Donald Trump na Urusi kuhusu uchaguzi wa Marekani, uliompelekea rais huyo kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Mwendesha mashtaka Robert Mueller ametoa uamuzi huo baada ya karibu miaka miwili ya uchunguzi.

Ripoti yake iliwasilishwa kwa Waziri wa Sheria siku ya Ijumaa. Siku ya Jumapili Machi 24 Waziri Bill Barr alitoa muhtasari wa kura nne. kwa maneneo machache, alimsafisha rais wa Marekani na timu yake kwa kutohusika na njama yoyote na Urusi wakati wa kampeni ya uchaguzi ya mwaka 2016.

Kuhusu madai ya kuwa pingamizi kwa sheria, Robert Mueller amemuachia waziri wa sheria nafasi ya kuamua kufungua mashtaka, na Waziri amehitimisha kwamba mashitaka hayahitajiki

Les quatre pages de synthèse issues du rapport Mueller et communiquées par le ministre de la Justice William Barr au Congrès, le 24 mars 2019.
Les quatre pages de synthèse issues du rapport Mueller et communiquées par le ministre de la Justice William Barr au Congrès, le 24 mars 2019. REUTERS/Jim Bourg

Ripoti hiyo inakamilisha uchunguzi wa miaka miwili wa Bwana Mueller, ambapo wakati wa uchunguzi huu washirika wa karibu wa rais walishitakiwa, na wakati mwingine hata kufungwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.