Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Maeneo kadhaa ya Venezuela yasalia bila umeme

Sehemu kubwa ya Venezuela, ikiwa ni pamoja na vitongoji kadhaa katika mji mkuu wa Caracas, vimeendelea kukumbwa na kiza kinene kufuatia kukatika kwa umeme.
Sehemu kubwa ya Venezuela, ikiwa ni pamoja na vitongoji kadhaa katika mji mkuu wa Caracas, vimeendelea kukumbwa na kiza kinene kufuatia kukatika kwa umeme. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Kiza kinene kimeyakumba maeneo mengi nchini Venezuela tangu Jumatatu usiku, ikiwa ni pamoja na vitongoji kadhaa vya mji mkuu Caracas, kutokana na kukatwa kwa umeme kwenye kituo cha nishati, kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la Habari la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii inakuja wiki mbili baada ya nchi hiyo kutumbukia katika kiza kinene kwa wiki kadhaa. Maeneo mengi ya mashariki na katikati ya mji mkuu, ambako kunapatikana ikulu ya rais, Miraflores, na wizara kuu yalikuwa hayana umeme.

Treni ya mwendo kasi inayotumia umeme ya mji mkuu Caracas imesitisha shughuli zake kwa sababu hali hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters, majimbo kadhaa, magharibi mwa nchi yamejikuta katika hali kama hiyo ingawa mji wa Puerto Ordaz kusini mwa Venezuela na baadhi ya maeneo ya Valencia, mji wa tatu kwa ukubwa, hayakukumbwa na hali hiyo.

Biashara zilifungwa mapema Jumatatu ili kuepuka uwezekano wa kuporwa iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari ya Venezuela, hali hiyo imesababishwa na shambulio dhidi ya bwawa kuu llinalozalisha umeme nchini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.