Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-BIASHARA

Rais Trump aendelea kushinikiza kuogeza ushuru kwa bidhaa kutoka Mexico

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Joshua Roberts

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika mazungumzo kati ya nchi yake na Mexico kuhusu uwezekano wa kuondoa vikwazo vya kibiashara alivyotangaza hivi karibuni, akitaka nchi hiyo idhibiti wimbi la wahamiaji.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, rais Trump amesema mazungumzo hayo yataendelea tena siku ya Alhamisi, hatua inayokuja wakati huu takwimu zikionesha kuwa idadi ya wahamiaji kutoka Mexico wanaoshikiliwa nchini humo imefikia kiwango cha juu kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 2006.

Katika mazungumzo ya juma hili, utawala wa rais Trump uliweka masharti magumu kwa Mexico ikiwa inataka iondolewe tozo kwenye bidhaa zake, utawala wa Washington ukitaka Mexico idhibiti wahamiaji wanaovuka mpaka.

Ikiwa mazungumzo ya juma hili yatagonga ukuta, inamaanisha kuwa tozo ya asilimia tano itaanza kutozwa na ifikapo October mosi, tozo hiyo itaongezeka hadi kufikia asilimia 25.

Trump anasema wahamiaji kutoka nchini Mexico wamekuwa hatari kwa usalama na uchumi wa taifa lake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.