Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC-USALAMA

Wapiganaji wa zamani 724 wa FARC watoroka

Tangu kuanza kwa mchakato wa amani, zaidi ya wapiganaji wa zamani 1,600 walijisalimisha na kuamua kuweka silaha chini kabla ya kujiunga na makundi mengine. Kwa mujibu wa serikali, wapiganaji hao wa zamani wako katika majimbo 12 kati ya 32 yanayounda Colomb
Tangu kuanza kwa mchakato wa amani, zaidi ya wapiganaji wa zamani 1,600 walijisalimisha na kuamua kuweka silaha chini kabla ya kujiunga na makundi mengine. Kwa mujibu wa serikali, wapiganaji hao wa zamani wako katika majimbo 12 kati ya 32 yanayounda Colomb LUIS ACOSTA / AFP

Wapiganaji wa zamani 724 wa kundi la zamani la waasi la FARC wametoroka, na kusababisha wasi wasi mkubwa kwamba wamejiunga na makundi mengine ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wa zamani 724 wangelishiriki katika zoezi nzima la kurejeshwa katika maisha ya kiraia kama ilivyoafikiwa katika makubaliano ya amani yaliyowekewa saini mwaka 2016 kati ya serikali ya Colombia na kundi la waasi wa zamani la FARC. Lakini "wameamua kutoroka," gazeti la kila siku la El Tiempo (linaloshapisha habari kwa Kihispania) limeripoti.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, zimekuwa wiki kadhaa sasa tangu tume ya mseto, inayojumuishwa na serikali, Umoja wa Mataifa na kundi la zamani la waasi la FARC, ambalo sasa limesajiliwa kama chama cha siasa, wakiwatafuta wapiganaji hao nchini kote, bila mafanikio.

Wapiganaji hao wa zamani 724 wote wamefundishwa kutumia silaha. Wasiwasi ni mkubwa kwamba wanaweza kujiunga na makundi haramu, baada tu ya viongozi kadhaa wa zamani wa kundi hilo pia kutoroka.

Serikali imetahadharisha jeshi, pamoja na serikali za majimbo kadhaa, hasa zinazokabiliwa na makundi ya yanayofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya na makundi mengine yanayobebelea silaha.

Tangu kuanza kwa mchakato wa amani, zaidi ya wapiganaji wa zamani 1,600 walijisalimisha na kuamua kuweka silaha chini kabla ya kujiunga na makundi mengine. Kwa mujibu wa serikali, wapiganaji hao wa zamani wako katika majimbo 12 kati ya 32 yanayounda Colombia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.