Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-BOLTON-SIASA

Trump amfuta kazi mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa

Mshauri wa Usalama wa taifa wa Marekani John Bolton wakati wa ziara yake London, Agosti 12, 2019.
Mshauri wa Usalama wa taifa wa Marekani John Bolton wakati wa ziara yake London, Agosti 12, 2019. REUTERS/Peter Nicholls

Rais wa Marekani Donald Trump amemuachisha kazi mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, John Bolton, kwa sababu ambayo wengi wanaona kwamba ni uhasama kati ya wawili hao.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo kadhaa vinabaini kwamba kumekuepo na tofauti kati yao. Donald Trump ameamua kuachana na mshauri wake wa usalama wa taifa John Bolton, na kumtaja, rafiki, kama kawaida yake, katika ukurasa wake wa twitter:

"Nilimfahamisha John Bolton kuwa hatuitaji huduma zake tena katika ikulu ya White House, " amesema Donald Trump.

John Bolton ni mshauri wa tatu wa usalama wa taifa ambaye anafukuzwa kazi katika kipindi cha miaka miwili na nusu.

"Sikukubaliana naye juu ya maswala mengi," ameongeza rais wa Marekani. Wakati John Bolton amezungumza mengine, tofauti na kauli ya Rais Donald Trump, akibaini kwamba ameamua mwenyewe kujiuzulu.

Kujiuzulu huku au kufutwa kazi huku, kunaonyesha jinsi gani utawala wa Trump unaendelea kukabiliwa na sintofahamu, katika mazingira magumu ya kidiplomasia na yenye utata.

Kwa wiki kadhaa, Washington imekuwa ikichukuwa hatua zinazotofautiana, haswa kwenye suala la Irani, kati ya hatua kali na utayari wa kuketi kwenye meza ya mazungumzo. Hatua ya kumuachisha kazi John Bolton pia inakuja saa 48 baada ya kufutwa kwa mkutano wa siri kati ya Washington na Taliban.

Trump hakukubaliana na mshauri wake wa usalama wa taifa katika masuala mengi. Hata hivyo John Bolton hakukubaliana na sera ya kiongozi wake ya kujisogeza karibu ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

John Bolton alimsihi kiongozi wake mara kadhaa kuacha kuzungumza na nchi yoyote adui wa Marekani, badala yake kufanya mashambulizi kwanza, kabla ya kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Donald Trump ameendelea kukosolewa kuhusu sera yake kwa wahamiaji.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.