Pata taarifa kuu
BOLIVIA-UCHAGUZI-SIASA

Bolivia: Evo Morales ashinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza

Rais wa Bolivia Evo Morales wakati wa mkutano na waandishi wa habari, ikulu, Oktoba 23, 2019.
Rais wa Bolivia Evo Morales wakati wa mkutano na waandishi wa habari, ikulu, Oktoba 23, 2019. REUTERS/Manuel Claure

Rais wa Bolivia anayemaliza muda wake Evo Morales ameshinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza, kulingana na matokeo ya awali ya mamlaka ya uchaguzi, baada ya asilimia 99.99 ya kura kuhesabiwa.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la uhesabuji wa kura linaendelea kuzua utata. Taasisi za kimataifa, kama vile OAS, zinahoji makosa kadhaa katika mchakato wa uchaguzi.

Kulingana na ukurasa wa Tovuti ya Mahakama Kuu ya Uchaguzi (TSE), Rais Evo Morales amepata asilimia 47.07 ya kura, dhidi ya asilimia 36.51 alizopata mpinzani wake mkuu, Carlos Mesa. Hiyo ni tofauti kubwa zaidi ya alama 10 zinazohitajika kushinda katika duru ya kwanza.

Evo Morales hakusubiri matokeo haya rasmi kabla ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi huu.

"Tumeshinda katika duru ya kwanza," Rais Evo Morales amesema, mbele ya waandishi wa habari Alhamisi wiki hii.

Rais Morales yuko madarakani tangu mwaka 2006 na anatarajia kuendelea kwa muhula wa nne mwaka 2020-2025. Hata hivyo mapema Alhamisi alitangaza kwamba kuna uwezekano ashiriki katika duru ya pili ya uchaguzi

"Ikiwa hatutashinda kwa alama 10, tutaheshimu" matokeo, "ikiwa tutatakiwa kushiriki katika duru ya pili, tutashiriki," alisema.

Mgombea mkuu wa upinzaji, Carlos Mesa, ambaye mwanzoni alitarajiwa kupambana na mshindani wake katika duru ya pili, amefutilia mbali matokeo ya uchaguzi na ameitisha katika siku zijazo maandamano ya amani kupinga udanganyifu huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.