Pata taarifa kuu
ARGENTINA-SIASA

Alberto Fernandez ashinda uchaguzi wa urais Argentina

Alberto Fernandez na mgombea mwenza, rais wa zamani Cristina Kirchner baada ya ushindi wao katika duru ya kwanza Oktoba 27 Buenos Aires.
Alberto Fernandez na mgombea mwenza, rais wa zamani Cristina Kirchner baada ya ushindi wao katika duru ya kwanza Oktoba 27 Buenos Aires. REUTERS/Agustin Marcarian

Baada ya 80% ya kura kuhesabiwa, Alberto Fernandez ametangazwa msindi wa uchaguzi wa urais dhidi ya rais anayemaliza muda wake, Mauricio Macri, ambaye tayari amempongeza mshindi.

Matangazo ya kibiashara

Alberto Fernandez, ambaye ni mgombea wa mrengo wa kushoto, ameshinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza, uliofanyika Jumapili Oktoba 27. Bw Fernandez amepata zaidi ya asilimia 47 ya kura, dhidi ya msindani wake, rais anayemaliza muda wake Mauricio Macri, ambaye amepata zaidi ya asilimia 41 ya kura.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani, zaidi ya 80% ya raia wa Argentina wamepiga kura.

Kufufua uchumi

Kuanzia Jumatatu wiki hii, udhibiti wa kubadilisha fedha za kigeni utaimarishwa, ili kupunguza ukomo wa kuporomoka kwa sarafu ya nchi hiyo, hali iliyosababisha dola bilioni 23 kupotea kutoka Benki Kuu tangu uchaguzi wa Agosti 11. Lengo: kuzuia nchi isijikuti haina akiba ya fedha Desemba 10, tarehe ya ambayo rais mpya anatarajiwa kukabidhiwa madaraka, mwandishi wetu Buenos Aires, Jean-Louis Buchet amebaini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.