Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

China na Marekani zatia saini sehemu ya 1 ya mkataba wa biashara

Naibu wa Waziri Mkuu wa China Liu He (kushoto) na Rais wa Marekani, Donald Trump (kulia) wakitia saini sehemu ya kwanza ya mkataba wa biashara kati ya Marekani na China.
Naibu wa Waziri Mkuu wa China Liu He (kushoto) na Rais wa Marekani, Donald Trump (kulia) wakitia saini sehemu ya kwanza ya mkataba wa biashara kati ya Marekani na China. SAUL LOEB / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump na Naibu wa Waziri Mkuu wa China Liu wametia saini sehemu ya kwanza ya mkataba wa biashara katika ikulu ya White House Jumatano, Januari 15.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo utasaidia mataifa hayo mawili kufanya biashara bila vikwazo.

Rais Donald Trump amesema mkataba huo, utasaidia sana kuimarisha uchumi wa Marekani, huku China ikisema ,ni mkataba ambao utayasaidia mataifa hayo mawili.

Hatua ya Donald Trump kusitisha vita vya biashara katika majira ya baridi mwaka 2018 hatimaye imezaa matunda.

Baada ya sherehe hiyo, waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin amebaini kwamba wamepata ushindi mkubwa katika sekta ya viwanda na kilimo nchini Marekani. Amesema pia kwamba wamefikia "hatua kubwa" na kubaini kwamba Marekani haijafikia kupunguza kodi kwa bidhaa kutoka China. "Hii itatokea tu ikiwa baada ya kutia saini sehemu ya pili ya mkataba," Steven Mnuchin amesema.

China imesema itaongeza bidhaa inayoingiza nchini Marekani kwa Dola Bilioni 200.

Naibu wa Waziri Mkuu wa China Liu amekaribisha "umuhimu wa mpango huo." Alisoma pia barua ndefu kutoka kwa Rais Xi Jinping aliyomtumia mwenzake wa Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.