Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SENATE-SIASA

Kamati ya Senate nchini Marekani kuanza kusikiliza mashtaka dhidi ya rais Trump

Maseneta nchini Marekani wanapojiandaa kusikiliza mashtaka dhidi ya rais Donald Trump 21.01.2020
Maseneta nchini Marekani wanapojiandaa kusikiliza mashtaka dhidi ya rais Donald Trump 21.01.2020 Jose Luis Magana/ Pool via REUTERS

Mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaomwakilisha katika kesi ya kumwondoa madarakani iliyo mbele ya Kamati ya Senate, wanataka kumalizika haraka kwa kesi hiyo na mteja wao kuondolewa madai yanayomkabili. 

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa Kamati hiyo, Mawakili wa Trump wanasema zoezi hilo ni hatari kwa katuba ya nchi ya Marekani.

Wakati huo, Maseneta wa chama cha Demoicratic nao pia wametoa taarifa yao na kudai kuwa Trump ameendelea kujihusisha na vitendo vinavyoonesha kuwa anataka kujuhusisha na udanganyifu wakati wa Uchagu Mkuu mwezi Novemba.

Kesi dhidi ya rais Trump ambaye anashatakiw akwa kutumia vibaya madaraka yake na kudharau mamlaka ya bunge inaanza siku ya Jumanne, na inakuja baada ya bunge la wawakilisha mwaka uliopita kupiga kura ya kukosa imani na kiongozi huyo kutoka chama cha Republican.

Kumwondoa  madarakani katika baraza hilo lenye Masenta 100, inabidi Maseneta 67 wabunge mkono hoja hiyo.

Chama cha Democratic ambacho kinashinikiza kuondolewa madarakani kwa rais Trump kina Maseneta 47.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.