Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Donald Trump ashtumiwa kudanganya kwa lengo la kuchaguliwa tena

Mwendesha Mashtaka Mkuu kutoka chama cha democratic Adam Schiff ameongoza mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump, Jumatano Januari 22, 2020.
Mwendesha Mashtaka Mkuu kutoka chama cha democratic Adam Schiff ameongoza mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump, Jumatano Januari 22, 2020. REUTERS/U.S. Senate TV

Wakati kesi ya ung'atuzi dhidi ya rais wa Marekani Donald trump ikiendelea kwa siku ya tatu, Waendesha mashitaka kutoka chama cha Democratic wamemshtumu rais huyo kuwa alijaribu kudanganya ili achaguliwe.

Matangazo ya kibiashara

"Trump alitumia vibaya madaraka ya ofisi yake kwa madhumuni ya kujiongezea nafasi ya kuchaguliwa tena, amesema Adam Schiff ambaye anaongoza mashtaka

"Ikiwa hajatiwa hatiani na Bunge la Seneti na kuvuliwa jukumu lake. Matumizi yake mabaya ya madaraka yatabadilisha kabisa usawa wa madaraka, " ameonya Adam Schiff.

Wademocrat wanamshutumu Trump kumshinikiza rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuanzisha uchunguzi dhidi ya makamu rais wa zamani Joe Biden, ambaye anaweza kuwa mpinzani wa Trump katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba mwaka huu.

Wanasema alitumia msaada wa kijeshi unaotolewa na Marekani kwa Ukraine wa kiasi cha dola milioni 391.

 

Hata hivyo Warepublican wanaendelea kuonyesha uungwaji wao mkono kwa rais Donald Trump.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.