Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Marekani yajiandaa kwa "hali mbaya" inayoweza kutokea

Donald Trump alionya kwamba Marekani inaingia katika kipindi "cha kutisha", Aprili 3, 2020.
Donald Trump alionya kwamba Marekani inaingia katika kipindi "cha kutisha", Aprili 3, 2020. REUTERS/Tom Brenner

Nchini Marekani, zaidi ya watu 300,000 wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao Umoja wa Mataifa umeutaja kuwa ni janga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ni nchi iliyoathirika zaidi ulimwenguni na janag hili la Covid-19. Zaidi ya watu 8,000 wamefariki dunia, kulingana ripoti ya Chuo Kikuu cha John Hopkins cha Baltimore. Na huko Washington, Donald Trump ameaonya raia wenzake: "Wiki hii itakuwa mbaya zaidi. "

Dunia kwa sasa inakabiliwa mgogoro wa kiafya kufuatia janga la Covid-19 na Marekani sasa inakabiliwa na hali ngumu kufuatia janga hilo.

Siku ya Jumamosi Aprili 4, Donald Trump alionya kwamba nchi yake itakabiliwa na "kipindi kigumu na cha kutisha". Virusi vya Corona vinasambaa haraka. "Kutakuwa na vifo vingi," aliongeza rais wa Marekani.

Marekani imekuwa sasa kitovu cha janga hili. Mgogoro wa kiafya ni mkubwa. Marekani ambayo ni miongoni mwa nchi zenye nguvu dunia imezidiwa na visa vya maambukizi na vifo kufutia ugonjwa wa Covid-19.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.