Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: China yatangaza visa vipya 62 vya maambukizi

Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi nchini China, hasa katika mji wa Wuhan, ambako ulianzia.
Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi nchini China, hasa katika mji wa Wuhan, ambako ulianzia. cnsphoto via REUTERS

Mamlaka ya afya nchini China imethibitisha visa vipya 62 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambapo janga hilo lilizuka mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Siku moja kabla watu 32 waliambukizwa virusi vya Corona, kwamujibu wa mamlaka ya afya.

Vifo viwili vya nyongeza vinavyohusiana na COVID-19 vimeripotiwa, Tume ya kitaifa ya afya imesema katika mkutano wake la kila siku na waandishi wa habari.

Kulingana na ripoti ya tume hiyo, visa 81,802 vya maambukizi na vifo 3,333 vimeripotiwa nchini China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo.

Wakati huo huo rais Donald Trump amelishukia shirika la afya duniani WHO na kulilaumu kwa kuegemea upande wa China.Trump amesema asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China kuficha ukweli kuhusu ugonjwa hatari wa Covid-1.

Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.