Pata taarifa kuu
CANADA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Hofu yatanda zaidi nchini Canada

Waziri wa Canada Justin Trudeau
Waziri wa Canada Justin Trudeau REUTERS/Chris Wattie

Ugonjwa wa Covid-19 unaweza kusababisha vifo hadi 22,000 nchini Canada na idadi ya visa vya maambukizi inaweza kuongezeka kutoka 934,000 hadi milioni 1.9 nchini humo, mamlaka ya afya imesema.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, amesema hali ya kawaida inaweza kurejea pale tu chanjo itaanza kutolewa, hali ambayo itachukuwa muda wa hadi miezi kumi na nane.

Wawakilishi wa mamlaka ya afya wamebaini kwamba matukio mawili yanayoweza kutokea kutokana na janga hili yanaonyesha kuwa kati ya watu 11,000 na 22,000 watafariki dunia kwa Covid-19 nchini humo.

Mkurugenzi wa afya, Theresa Tam, amesema ni muhimu raia waendelee kubaki nyumbani.

"Ingawa data zilizotolewa leo zinaweza kuonekana kuwa mbaya, tathmini kwa Canada inaonyesha kuwa nchi hii bado ina nafasi ya kudhibiti janga hili," Theresa Tam alisema Alhamisi wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari.

Naibu wake, Howard Njoo, alibaini kwamba ikiwa mambo yatakwenda vizuri wimbi la kwanza la janga hilo linaweza kumalizika hadi mezi Julai au Agosti. Lakini ameongeza kwamba baadaye kutakuwa na mawimbi madogo ya milipuko ho wa Covid-19.

Serikali za mkoa nchini kote Canada zimeagiza kufungwa kwa biashara ambazo sio muhimu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19, na kusababisha mamilioni ya watu kupoteza kazi. Kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Alhamisi wiki hii, zaidi ya watu milioni moja walipotea ajira nchini Canada mwezi Machi mwaka huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.