Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Msemaji wa makamu wa rais wa Marekani apatikana na virusi vya Corona

Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 75,000.
Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 75,000. REUTERS/John Sommers II

Msemaji wa Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ambaye mke wa mmoja kati ya washauri wakuu wa Donald Trump, amethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, hali ambayo inazua wasiwasi wa kusambaa kwa virusi hivyo katika ikulu ya White House.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani mwenyewe alitangaza siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na wabunge na maseneta kutoka chama cha Republican kwamba Katie Miller, mke wa mshauri wake wa katika masuala ya uhamiaji, Stephen Miller, ameathirika.

Kesi nyingine iliripotiwa siku moja kabla kati ya wafanyakazi wa White House wanaomhudumia rais Trump.

Kulingana na mjumbe mashuhuri wa utawala wa Marekani, akinukuliwa na waandishi wa habari, Donald Trump na Mike Pence hivi karibuni hawakuweza kukaribiana na Katie Miller.

Kutangazwa kwa kesi hii ya pili kwa siku mbili katika Ikulu ya White House kumezua hofu kwa afya ya rais na makamu wa rais, ambao wote wawili walianza tena shughuli zao na safari zao, wakati vifo vya watu waliofariki kwa Covid-19 vimezidi 75,000.

"Tumechukua tahadhari zote kumlinda rais," amesema Kayleigh McEnany, msemaji wa ofisi ya rais, Ijumaa wiki hii. "Tumefanya kile ambacho Dk.(Deborah) Birx na Dk(Anthony) Faucie walituomba amesema.

Donald Trump na Mike Pence wote wamepimwa na hawajapatikana na virusi vya Corona hasa baada ya afisaa mmoja wa jeshi la Marekani anayehudumu katika Ikulu ya White House kuthbitishwa kuwa na virusi, ofisi ya rais aw Marekani imesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.