Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus-Trump: Ninatathmini uwezekano wa kupunguza mawasiliano yangu na Pence

Rais wa Marekani Donald Trump awali alilishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China, baada ya kusema kuwa walipuuzia kuhusu hatari ya ugonjwa wa Covid-19..
Rais wa Marekani Donald Trump awali alilishutumu shirika la Afya Duniani, WHO, kwa kuipendelea China, baada ya kusema kuwa walipuuzia kuhusu hatari ya ugonjwa wa Covid-19.. REUTERS/Tom Brenner

Rais wa Marekanio Donald Trump amebaini kwamba anatahmini uwezekano wa kuzuia mawasiliano yake na Makamu wake Mike Pence ambaye alionekana akithibitisha kwamba yuko karantini baada ya msaidizi wake kupatikana na virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua za kupunguza mawasiliano yao kwa kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona, rais wa Marekani amejibu: "Hili ni jambo ambalo labda tutazungumzia katika kipindi hiki cha kizuizini".

Mike Pence, ambaye anaongoza kikosi kazi cha rais Trump kinachopambana na maambukizi ya virusi vya corona, hakuwepo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.

Wakati huo huo wataalamu wa juu wa masuala ya afya wa utawala wa rais Donald Trump wa Marekani wanaohusika na janga la virusi vya corona watatoa ushahidi katika Baraza la Seneti kwa njia ya vidio wiki hii baada ya watatu kati yao pamoja na mwenyekiti wa kamati kukaribiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya COVID-19.

Hayo yanajiri wakati idadi ya vifo vinavyotokana na janga la Corona imefikia zaidi ya 80,000 nchini Marekani, kulingana na takwimu za shirika la habari la Reuters.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.