Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA

Covid-19 yaua zaidi ya watu 82,000 nchini Marekani

Watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona, na zaidi ya watu milioni 4.3 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona.
Watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona, na zaidi ya watu milioni 4.3 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona. REUTERS

Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) vimetangaza vifo vipya 1,426 vinavyohusiana na Corona, na kufikisha jumla ya watu 82,246 waliofariki dunia tangu kuzuka kwa janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

ituo vya CDC pia vimeripoti visa vipya 21,647 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, na kufikisha jumla ya idadi ya visa 1,364,061 vya maambukizi nchini humo.

Watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona, na zaidi ya watu milioni 4.3 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani limeyataka mataifa kuchukua tahadhari za hali ya juu.

Katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya Corona vitatoweka.

"Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na virusi hivi huenda visiishe, " Dkt Mike Ryan amesema.

Hayo yanajiri wakati Ulaya imeanza kuchukua hatua za awali kuelekea kufungua mipaka yake ya ndani, baada ya miezi miwili ya vizuizi vya kukabiliana na janga la Covid-19, huku WHO ikiyataka mataifa kuchukua tahadhari za hali ya juu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.