Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA-SIASA

Trump amfukuza kazi mkuu wa serikali anayemchunguza Pompeo

Idara ya serikali imetangaza kwamba nafasi ya Steve Linick itachukuliwa na Stephen Akard, mkurugenzi wa sasa wa ofisi ya masuala ya kigeni.
Idara ya serikali imetangaza kwamba nafasi ya Steve Linick itachukuliwa na Stephen Akard, mkurugenzi wa sasa wa ofisi ya masuala ya kigeni. Reuters

Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Mkaguzi Mkuu wa serikali Steve Steve Linick, uamuzi uliokosolewa na upinzani kutoka Chama cha Democratic ambao wamebaini kwamba afisa huyo mwandamizi alikuwa ameanzisha uchunguzi dhidi ya waziri wa Mambo ya Ndani Mike Pompeo.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi, ambaye ni kutoka Chama cha Democratic, rais Donald Trump amebaini kwamba Steve Linick hana imani tena, bila kutaja sababu.

Steve Linick, ambaye aliteuliwa mnamo mwaka 2013 chini ya utawala wa Barack Obama, ataachia ngazi ndani ya siku 30 zijazo, ameongeza Donald Trump katika barua yake.

Idara ya serikali imetangaza kwamba nafasi ya Steve Linick itachukuliwa na Stephen Akard, mkurugenzi wa sasa wa ofisi ya masuala ya kigeni.

Kulingana na mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya nje katika Baraza la Wawakilishi, Eliot Engel, kutoka chama cha Democratic, "ofisi ya Mkaguzi Mkuu ilifungua uchunguzi kuhusu Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo". Engel hajaeleza sababu ya uchunguzi huo.

Nancy Pelosi amelaani "mfumo hatari wa kulipiza kisasi" wa Donald Trump, ambaye tayari ameshawafukuza wakaguzi wengine kadhaa katika wiki za hivi karibuni.

Mwanzoni mwa mwezi Mei, rais wa Marekani alimuachisha kazi Christi Grimm, aliyekuwa mkuu wa ofisi ya ukaguzi mkuu kwenye wizara ya afya, akimshtumu kufanya "faili ya uwongo" kuhusu uhaba wa hospitali zinazokabiliana dhidi ya janga la Corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.