Pata taarifa kuu
GUATEMALA-EL SALVADOR-KIMBUNGA-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Amanda chapiga Guatemala, 14 wafariki dunia El Salvador

Eneo jirani na San Salvador limeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu kutokana na kimbunga Amanda, Mei 31, 2020.
Eneo jirani na San Salvador limeendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu kutokana na kimbunga Amanda, Mei 31, 2020. AFP

Kimbunga Amanda, ambacho ni cha kwanza kwa msimu huu katika Bahari ya Pasifiki, kimepiga nchini Guatemala na El Salvador Jumapili Mei 31, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 14 nchini El Salvador, nchi ambayo imetangaza hali ya dharura.

Matangazo ya kibiashara

Kimbunga Amanda kimeendelea kupiga tangu Jumamosi katika Pwani ya Guatemala na kimesababisha hali ya mbaya hewa katika nchi hizo mbili za Amerika ya Kati, huku mito ikifurika maji na kusababisha umeme kukata.

Kutokana na hatari ya kutokea maporomoko ya udongo, Rais wa El Salvador Nayib Bukele ametangaza hali ya hatari kwa siku 15 muda, ambao unaweza kuongezwa.

"Tunakabiliwa na hali ngumu (...) tumepoteza watu 14" na "idadi hii inaweza kuongezeka", Waziri wa Mambo ya Ndani wa El Salvador, Mario Duran amesema.

Watu kumi wamefariki dunia katika mji mkuu San Salvador na vitongoji vyake na watu watatu kutoka familia moja wamefariki dunia huko San Juan Opico katika eneo La Libertad, katikati mwa nchi, kwa mujibu wa mamlaka. Wakati huo huo, mtu mmoja mtu mmoja hajulikani aliko katika mji wa San Salvador.

Huko San Salvador, karibu watu 4,200 wamepewa hifadhi kwenye makazi yaliyotengwa na idara inayokabiliana na majanga baada ya nyumba zao kusombwa na maji au au wale waliohamishwa, kulingana na meya wa mji mkuu, Ernesto Muyshondt.

"Tunaishi katika hali isiyo ya kawaida, dharura kubwa ambayo inakuja kujiongeza kwa dharura nyingine kubwa, ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia," amesema Muyshondt, akimaanisha janga la Corona.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.