Pata taarifa kuu
INDIA

Daktari mwanafunzi aliyebakwa nchini India afariki dunia

Hospitali ya Mount Elizabeth ya nchini Singapore alikokuwa akitibiwa mwanamke aliyebakwa nchini India
Hospitali ya Mount Elizabeth ya nchini Singapore alikokuwa akitibiwa mwanamke aliyebakwa nchini India haveeru.com.mv

Madaktari katika hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore wametangaza kuwa mwanamke aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia kubakwa na kundi la wanaume sita mjini New Delhi nchini India amefariki dunia. 

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo za simanzi zinaeleza kuwa mwanamke huyo daktari mwanafunzi,ambaye tukio la kubakwa kwake lilizusha maandamano makubwa nchini mwake, amefariki kwa amani mapema asubuhi leo Jumamosi.

Akielezea kwa masikitiko taarifa hizo mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Kelvin Loh amesema kuwa pamoja na jitihada zote zilizofanywa na timu ya wataalamu sita kuhakikisha kuwa hali yake inaimarika, juhudi hizo zimegonga mwamba na hatimaye majira ya saa 10 na dadika 45 alfajiri hii leo amefariki dunia.

Kufuatia taarifa za kifo hicho waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa hizo na kuahidi kuchukua hatua madhubuti dhidi ya waliotekeleza unyama huo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.