Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq: jeshi laanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya ISIL

Mmoja kati ya wanajeshi wa Iraq akiwa ndani ya helikopta akichunguza ngome za wapiganaji wa makundi ya kiislamu yaliyounda hivi karibuni taifa la kiislamu.
Mmoja kati ya wanajeshi wa Iraq akiwa ndani ya helikopta akichunguza ngome za wapiganaji wa makundi ya kiislamu yaliyounda hivi karibuni taifa la kiislamu. REUTERS/Stringer

Ndege za kivita za Iraq zimeanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa makundi ya wapiganaji wa kiislamu wanaoshikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq, ikiwemo eneo la Washia la Amerli, ambako raia wanakabiliwa na uhaba wa maji.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wameendelea kuteka baadhi ya maeneo katika mataifa ya Iraq na Syria, huku Umoja wa mataifa ukinyooshea kidole makundi hayo kuhusika na vitendo viovu dhidi ya raia hususan kuua hadharani watu wasiyokua na hatia.

Hata hivo nchi yumkini 9 zimekubali kuwapa silaha wapiganaji wa kikurdi ili waendeleye kupambana dhidi ya wapiganaji hao wa akiislamu.

Hayo yakijiri, kwa mujibu wa New York Times, rais wa Marekani Barack Obama iko mbioni kuchukua hatua kuhusu mashambulizi nchini Syria na amekua akitafakari namna ya kuunda mmungano wa kikosi cha kimataifa cha kuweza kusambaratisha makundi hayo ya wapiganaji wa kiislamu.

Marekani ambayo ilianza kutuma ndege ya kufanya uchunguzi nchini Syria, imeendesha tangu Agosti 8 mwaka 2014 mashambulizi ya anga ikisaidia wapiganaji wa kikurdi dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kiislamu nchini Iraq.

Afisa mmoja wa jeshi la Iraq amesema kwamba ndege za kivita za Iraq zimeendesha mashambulizi 9 dhidi ya ngome za wapiganaji wa kiislamu.

Waziri wa Marekani mwenye dhamana ya ulinzi, Chuk Hagel, amebaini kwamba nchi nane, ikiwa ni pamoja na Marekani, Albania, Canada, Croatia, Denmark, Italia, Ufaransa na Uingereza, ziko tayari kuwapa silaha wapiganaji wa kikurdi. Kwa upande wake rais wa Kurdistan amebaini kwamba Iran ni nchi ya kwanza ambayo ilianza kuwapa silaha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.