Pata taarifa kuu
INDONESIA-Usalama wa Anga

AirAsia QZ8501:hali ya hewa yatatiza utafiti

Zoezi la anga la kuitafuta ndege ya shrika la Air Asia nchini Indonesia lasitishwa kutokana na mvua kubwa na upepo mkali Jumatano hii Desemba 31.
Zoezi la anga la kuitafuta ndege ya shrika la Air Asia nchini Indonesia lasitishwa kutokana na mvua kubwa na upepo mkali Jumatano hii Desemba 31. REUTERS/Edgar Su

Juhudi bado zinaendelea kutafuta miili zaidi baada ya kupatikana kwa mabaki ya ndege ya AirAsia jana Jumanne Desemba 30.

Matangazo ya kibiashara

Ndege ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia Jumapilli Desemba 28 mwaka 2014 iliyopita ikiwa na abiria 162.

 

Maafisa wa Indonesia wamethibitsiha kuwa mabaki yaliyopatikana yamedhirisha kuwa ni ya ndege hiyo ambayo imekuwa ikitafutwa tangu siku ya Jumapili katika Bahari ya Java.

Siku ya Jumanne iliripotiwa kuwa miilii 40 ilikuwa imepatikana baada ya kuonekana ikielea majini lakini maafisa wa jeshi la Maji nchini humo wamenukuliwa wakisema miili sita tu ndio iliyopatikana.

Rais wa Indonesia, Joko Widodo, amehidi kuwa waokoaji wanafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuhakikisha kuwa miili ziadi inapatikana.

Kwa sasa waokoaji wakitumia meli na ndege wanaendelea kutafuta miili zaidi na mabaki zaidi ya ndege hiyo iliyotoweka ikielekea Singapore ikitokea Indonesia.

Matiafa ya Marekani, China, Australia na Singapore yanasaidia upatikanaji kwa miili hiyo na mabaki ya ndege hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.