Pata taarifa kuu
VATICAN-PAPA-PAPA FRANCIS-SRI LANKA

Papa Francis ziarani Sri lanka

Papa Francis wakati wa sla yake ya kila siku, Januari 4 mwaka 2015.
Papa Francis wakati wa sla yake ya kila siku, Januari 4 mwaka 2015. REUTERS/Alessandro Bianchi

Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amewatolea wito viongozi wa Sri-Lanka wa kuheshim haki za binadamu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wito huo umetolewa na Kiongozi huyo mkuu wa Kanisa katoliki baada ya kuwasili nchini Sri Lanka hii leo Jumanne, chini ya wiki moja baada ya rais aliyekuwapo madarakani kwa muda mrefu nchini humo kushindwa katika uchaguzi.

Jamii ndogo ya waumini wa madhehebu ya Katoliki nchini humo inatarajia kwamba anaweza kusaidia kuponya majeraha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 25 nchini humo.

Vita kati ya waasi wa Tamil Tigers ambao ni wachache nchini humo, ambao wengi wao ni Wahindu, na serikali kuu, inayomilikiwa na jamii yenye watu wengi ya Sinhala, ambao ni Wabuddha, ilimalizika mwaka 2009.

Wakatoliki ni chini ya asilimia 7 nchini Sri Lanka, lakini ni kutoka makabila yote Watamil na Wasinhala, na kuwafanya kuwa daraja muhimu baina ya pande hizo mbili.
Baada ya Sri Lanka, Papa Francis atatembelea nchi ya Colombo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.