Pata taarifa kuu
SRI LANKA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wafanyika Sri Lanka

Katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Sri Lanka, Mei mwaka 2009.
Katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Sri Lanka, Mei mwaka 2009. (Photo : AFP)

Kura zimeanza kupigwa nchini Sri Lanka, huku rais wa zamani Mahinda Rajapaksa akitarajia kurudi uongozini kama Waziri mkuu.

Matangazo ya kibiashara

Kinyanga'nyiro ni kati ya chama cha Freedom Party cha rais huyo wa zamani na kile cha aliyekuwa Waziri mkuu Ranil Wickreme Singhe wa chama cha UNP.

Rajaspaka anatumai kuwa chama chake kitashinda ili awe Waziri mkuu baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais mapema mwaka huu dhidi ya Waziri wake wa afya Maithripala Sirisena.

Wachunguzi wa uchaguzi huu wanasema watu wanne wameuawa katika machafuko ya kisiasa huku kukiropitiwa matukio machache ya macjafuko ikilinganishwa na miaka iliyopita .

Watu milioni 15 wamesajiliwa kupiga kira na matokeo yanatarjiwa kufahaika kesho Jumanne.

Rajapaksa anayefahamika kwa kuwanyamazisha waasi wa Tamil baada ya kuisumbua serikali kwa miaka 26 amesema ana matumaini ya chama chake kushinda lakini chama cha rais Sirisena kimesema hakitakubali hicho kutokea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.