Pata taarifa kuu
URUSI-MISRI-AJALI YA NDEGE

Ajali ya ndege ya Urusi Misri: Urusi yaomboleza

Ndugu wa wahanga kwenye uwanja wa ndege wa St Petersbourg wakiweka shada za maua na mishumaa kwa heshima za watu waliopoteza maisha katika ajali ya ndege.
Ndugu wa wahanga kwenye uwanja wa ndege wa St Petersbourg wakiweka shada za maua na mishumaa kwa heshima za watu waliopoteza maisha katika ajali ya ndege. Reuters

Machozi, mishumaa na maua vimeshuhudiwa katika uwanja wa ndege wa St Petersburg Jumapili Novemba 1. Wakati huo huo Misri imeanzisha uchunguzi wa kujua kiini cha ajali hiyo, huku zoezi la kuhifadhi milii ya waliopoteza maisha ikianzishwa.

Matangazo ya kibiashara

Urusi iko katika maombolezo baada ya ajali ya ndege yenye chapa A321 ya shirika la Urusi la Metrojet, Jumamosi, Oktoba 31, katika Jangwa la Sinai nchini Misri. Idadi kubwa ya watu 224 waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni raia wa Urusi.

Maua na mishumaa vyawekwa kwa heshima ya wahanga

Mbele ta uwanja wa ndege wa St Petersburg, ambapo ndege hiyo ingelitua michumaa na maua vimewekwa kwa kutoa heshima kwa marehemu. Picha za waliopoteza maisha katika ajali hiyo zimewekwa kwenye eneo hilo na ndugu zao, huku zikizungukwa na maua pamoja na mishumaa. wato 17 ni miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea katika jangwa la Sinai. " Nataka kutoa rambirambi zangu kwa wote ndugu na marafiki wa watu waliopteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea nchi Misri ", amesema mkazi mmoja wa St Petersburg, aliyekuja kuweka maua.

Hisia ni kubwa wakati ambapo baadhi ya ndugu wa marehemu walikuwa njiani kwenda kuwatafuta wakati walipata taarifa ya tukio hilo la kusikitisha. Kwa kuwasaidia, kitengo cha kisaikolojia kimewekwa na mamlaka ili kuwahudumia wale ambao watakumbwa na tatizo lolote kutokana na hali hiyo.

Jumapili Novemba 1 ilitangazwa siku ya kitaifa ya maombolezo nchini Urusi, na Rais Vladimir Putin. Kwa hiyo, bendera imepandishwa nusu mlingoti. Kwenye runinga mbalimbali, programu zote za burudani zimefutwa, na picha za watu waliopoteza maisha katika jali hiyo zimekua zikirushwa hewani.

Jumamosi, Oktoba 31, saa 11:51 alfajiri, ndege yenye chapa A321 ya shirka la ndege la Urusi la Metrojet ilipaa angani kutoka uwanja wa ndege wa Sharm el Sheikh kwenda St Petersburg. Muda wa dakika ishirini baadaye, maafisa wa uwanja wa ndege waliopotea mawasiliano na rubani wa ndege, alipokuwa angani katika jangwa la Sinai. Watu 224 waliokua katika ndegewalipoteza maisha katika ajali hiyo. Kulingana na afisa wa Urusi, injini za ndege zilizima ndege ikiwa angani.

Hata hivyo kundi la Islamic State lilikiri Jumamosi Oktoba 31, baada ya kutokea ajali hiyo kuwa lilihusika katika udunguwaji wa ndege ya Urusi, katika hali ya kulipiza kisasi kufuatia operesheni inayoendeshwa na jeshi la Urusi kwa ushirikiano na jeshi la Syria dhidi ya ngome zao nchini Syria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.