Pata taarifa kuu
URUSI-MISRI-AJALI YA NDEGE

Miili 162 ya ajali ya ndege yasafirishwa Urusi

Mabaki ya ndege A321 katika eneo la Wadi al-Zolomat katika Rasi ya Sinai, Novemba 1, 2015.
Mabaki ya ndege A321 katika eneo la Wadi al-Zolomat katika Rasi ya Sinai, Novemba 1, 2015. KHALED DESOUKI/AFP

Ndege iliyoibeba miili 162 kati 224 ya watu walipoteza maisha katika ajali ya ndege ya shiria la Urusiimeondoka Cairo Jumapili hii, wakati ambapo uchunguzi wa kujua kiini cha ajali hiyo nazoezi la kutafuta miili ikiendelea nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo cha uwanja wa ndege mjini Cairo na msemaji wa Wizara ya dharura nchini Urusi, ndege inayobeba miili 162 imeondoka Cairo Jumapili hii jioni ikiwa njiani ikielekea St Peterburg, ambapo ndege hiyo aina ya 76 ilikua ikisubiriwa kutua saa 8:00 usiku saa za kimataifa.

Katika ajali hiyo ya ndege iliyotokea Jumamosi katika eneo la Sinai watu wote mia mbili na ishirini na nne walikuwa katika ndege hiyo walikufa.

Mmoja wa wachunguzi wa maswala ya anga kutoka Urusi amesema kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika jangwa la Sinai nchini Misri ililivunjika ikiwa hewani.

Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakanaa katika jangwa la Sinai.

Abiria wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo ,ambao idadi kubwa ni raia wa Urusi,wamefariki dunia, naye mchunguzi kutoka nchini Urusi amesema kwamba ni mapema mno kutaja chanzo cha ajali hiyo.

Jumapili usiku malfu kadhaa ya watu walitoa heshima zao katika mji wa pili wa Urusi kwa abiria 217 na wafanyakazi 7 wa ndege hiyo waliopoteza maisha katika ajali hiyo. Watu wote waliokua wakisafiri nandege hiyo ni kutoka Urusi isipokuwa watu watatukutoka Ukraine. Hii ni ajali mbaya ambayo imeikumba nchi ya Urusi.

Wakati huo huo Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi ametaka watu wote wawe na uvumilivu wakati uchunguzi ukiwa unaendelea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.