Pata taarifa kuu
URUSI-MISRI-AJALI YA NDEGE

Miili ya ajali ya ndege yapokelewa Urusi

Msafara wa magari yaliobeba miili ya baadhi ya watu 224 waliuawa katika ajali ya ndege ya Urusi iliyotokea Misri, ukiondoka Novemba 2, 2015 katika uwanja wa ndege wa Pulkovo.
Msafara wa magari yaliobeba miili ya baadhi ya watu 224 waliuawa katika ajali ya ndege ya Urusi iliyotokea Misri, ukiondoka Novemba 2, 2015 katika uwanja wa ndege wa Pulkovo. VASILY MAXIMOV/AFP

Ndege iliyobeba miili ya baadhi ya watu 224 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya shirika moja la Urusi nchini Misri Jumamosi Oktoba 31 imewasili Jumatatu hii katika mji wa St Petersburg, wakati ambapo uchunguzi wa kujua kiini cha ajali hiyo ukiendelea.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Wizara ya dharura ya Urusi, miili 144 ya watu waliopoteza maisha wakati ndege ya shirika moja la Urusi ilipoangiuka katika jangwa la Sinai nchini Misri. Jumapili jioni, chanzo cha uwanja wa ndege kilisema kuwa ndege moja ilisafirisha miili 162 nchini Urusi.

Msafara wa magari unatazamiwakuipeleka miili hiyo katika chumba cha kuhifadhi maiti cha St Petersburg (Kaskazini Magharibi mwa Urusi) kwa zoeli la kuitambua, kwa mujibu wa wizara ya dharura.

Kwa rahisisha zoezi hilo la kuitambua miili, familia za watu waliopteza maisha katik aajali hiyo zimetoa sampuli za DNA katika kituo kimoja, karibu na uwanja wa ndege, ambapo kumetengwa eneo kutakapofanyika sherehez aza kutoa heshima kwa marehemu hao, ikiwa ni pamoja na watoto 17.

Abiria wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo ,ambao idadi kubwa ni raia wa Urusi,wamefariki dunia, naye mchunguzi kutoka nchini Urusi amesema kwamba ni mapema mno kutaja chanzo cha ajali hiyo.

Jumapili usiku malfu kadhaa ya watu walitoa heshima zao katika mji wa pili wa Urusi kwa abiria 217 na wafanyakazi 7 wa ndege hiyo waliopoteza maisha katika ajali hiyo. Watu wote waliokua wakisafiri nandege hiyo ni kutoka Urusi isipokuwa watu watatukutoka Ukraine. Hii ni ajali mbaya ambayo imeikumba nchi ya Urusi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.