Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Japan na Marekani kupambana dhidi ya Korea Kaskazini

Meli kubwa ya kijeshi ya Marekani Nimitz ikiegesha kwenye bahari ya Hong Kong, Februari 17, 2010.
Meli kubwa ya kijeshi ya Marekani Nimitz ikiegesha kwenye bahari ya Hong Kong, Februari 17, 2010. Reuters/Bobby Yip

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley ameionya Korea Kaskazini na kusema muda wa mazungumzo kuhusu Korea Kaskazini umekwisha.

Matangazo ya kibiashara

Haley amesema hakuna sababu ya kuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo hakutakuwa na matokeo, yatakayoipa mbinyo Korea Kaskazini, huku akibaini kwamba China inatakiwa msimamo kama itaamua kuchukua hatua hii muhimu.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema yeye pamoja na rais wa Marekani Donald Trump wamekubaliana kuwa upo umuhimu wa kupambana na Korea ya Kaskazini katika mipango yake ya majaribio ya makombora.

Abe amewaambia waandishi wa habari kuwa anashukuru kujitolea kwa Rais Trump katika suala la Korea ya Kaskazini.

Mwishoni mwa juma hili lililopita rais wa Marekani Donald Trump alikosoa China kwa kukosa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inasitisha mipango yake ya silaha za nukia.

Maoni yake yalichapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatua kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.

Korea Kaskazini ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.