Pata taarifa kuu
JAPAN-KOREA KASKAZINI-UCHAGUZI-USALAMA

Shinzo Abe: Niko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika makao makuu ya chama chake, LDP, Tokyo, Oktoba 22, 2017.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika makao makuu ya chama chake, LDP, Tokyo, Oktoba 22, 2017. REUTERS/Kim Kyung-Hoon

Baada ya muungano wake kupata ushindi wa theluthi mbili ya viti vya bunge, Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema yuko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu unampa Shinzo. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.

Mapema wiki iliyopita Waziri mkuu Shinzo Abe alitoa wito wa kutaka jeshi la Japan lifanyiwe marekebisho, huku akibaini kwamba kunahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.

Awali Bw. Abe alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anataka kukifanyia mabadiliko kipengele cha katiba kinachozuia vita na kupelekea kutambuliwa kwa jeshi la Japan.

Miaka miwili iliyopita Bw Abe alifanikiwa kubadilisha katiba ambayo iliruhusu wanajeshi kupigana vita nje hatua ambayo ilipingwa vikali.

Shinzo Abe aliitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, ikiwa ni pamoja na tisho kutoka Korea Kaskazini.

Vyombo vya habari vimearifu kuwa muungano wa chama tawala cha Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) na chama cha Komeito ulishinda viti 312 kati ya viti 465 katika bunge la chini, ushindi unaoupa muungano huo nguvu za kubadilisha katiba.

Umaarufu wa Bw Abe ulishuka miezi miili iliyopita baada ya kushtumiwa katika visa mbalimbali , lakini umaarufu wake ulianza kupanda baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili kupitia anga ya Japan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.