Pata taarifa kuu
INDIA-USALAMA

Watu 15 wapoteza maisha Bombay, India

India yaendelea kukumbwa na majanga ya moto
India yaendelea kukumbwa na majanga ya moto CAPTURE INDIA NOW

Watu wasiopungua 15 wameangamia usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya jengo la makazi kuteketea kwa moto mjini Bombay, nchini India wakati wa sherehe.

Matangazo ya kibiashara

Moto huo ulianza muda mfupi baada ya usiku wa manane katika mgahawa wa ghorofa ya juu kabla ya kuenea haraka kwa baa mbili zilizo karibu, na kuharibu jengo lote kwa muda wa nusu saa, kulingana na ripoti mbalimbali za vyombo vya habari.

Wengi wa waathirika ni wanawake waliokua wakihudhuria sherehe katika mgahawa moja katika jengo hilo, Idara ya kukabiliana na majanga nchini humo.

"Mpaka sasa, vifo 15 vimeorodheshwa," S. Jaykumar, Mkuu wa polisi katika mji Bombay amewaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kujua chanzo cha moto huo. Zaidi ya watu kumi wamelazwa hospitalini, wawili kati yao wako katika hali mbaya.

Rais wa India Ram Nath Kovind ametoa rambi rambi zake kwa familia kwenye ukurasa wake wa Twitter. Ajali kama hizo zimekua zikitokea nchini India kutokana na sheria dhaifu za kiusalama na ukosefu wa udhibiti. Wiki chache iliyopita, moto uliuawa wafanyakazi 12 wakati walipokua wakilala.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.