Pata taarifa kuu
ISRAEL-INDIA-USHIRIKIANO

Benjamin Netanyahu azuru India

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. REUTERS/Sebastian Scheiner/Pool

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anazuru India kwa ziara ya siku sita. Netanyahu na mwenyeji wake Narendra Modi watajadiliana kuhusu maswala ya kibiashara, usalama na namna ya kuendeleza mshikamano wa nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Anakuwa Waziri Mkuu wa pili wa Israel kuzuru India baada ya nchi hizo mbili kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia mwaka 1992.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya India Raveesh Kumar kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema ziara hii inaadhimisha ushirikiano wa karibu wa miaka 25 kati ya India na Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasili katika mji mkuu wa India, New Delhi siku ya Jumapili katika ziara ya siku sita, ambapo ana matumaini ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kujadili tofauti zinazohusiana na hatua ya New Delhi kusitisha mkataba wa ulinzi, wametangaza maafisa wa nchi hizi mbili.

Januri 3 mwaka huu, Rafael, Kampuni ya Israel inayotengeneza vifaa vya kijeshi, ilitangaza kwambaIndia ilifuta mkataba wa mauzo ya makombora aina ya Spike kutoka India yenye thamani ya dola milioni 500 millions.

"Kama kuna tatizo, kuna uwezekano wa kulitatua", almesema Daniel Carmon, balozi wa Israel nchini India, akimaanisha kufutwa kwa mkataba wa ulinzi.

India ni soko kubwa la silaha la Israel, pamoja na mauzo ya silaha ya takriban dola bilioni 1 kila mwaka. Pamoja na kufutwa kwa mkataba huu wa makombora, hivi karibuni wizara ya ya ulinzi ya India ilitangaza kwamva iliidhinisha mpango wa dola milioni 72 wa kununua makombora 131 aina ya Barak yanayotengenezwa na kampuni ya Israel ya Rafael.

Nchi hizo mbili zimerejesha uhusiano wao tangu Narendra Modi achukuwe nafasi ya Waziri Mkuu wa India mwaka 2014, na hivyo kupanua ushirikiano wa biashara mbali na mahusiano yao ya ulinzi wa muda mrefu.

Netanyahu ameandamana na wajumbe 130 kutoka sekta za teknolojia, kilimo pamoja na ulinzi. Mbali na New Delhi, watatembelea Mumbai na Gujarat, mjimbo alikozaliwa Modi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.