Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-KOREA KUSINI

Bunge la Korea Kaskazini kuketi mwezi ujao kujadili yanayojiri

Screenshot ilichukuliwa tarehe 8 Februari 2018 ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.
Screenshot ilichukuliwa tarehe 8 Februari 2018 ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un. KCTV / AFP

Bunge linalofanya maamuzi nchini Korea Kaskazini linatarajiwa kufanya kikao chake cha kila mwaka mwezi ujao, huku macho yote yakielekezwa kuona ikiwa bunge hilo litaunga mkono mazungumzo yaliyoanza kupigiwa chapuo kati yake na Marekani na Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Juhudi za mazungumzo ya kidiplomasia ambazo zilianza kushuhudiwa wakati wa michezo ya majira ya baridi ya Olimpiki, zimeshuhudia rais wa Marekani Donald Trump akikubali kuwa na mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Bunge hili ambalo ndio hufanya maamuzi, hukutana mara moja au mbili kwa mwaka kuidhinisha bajeti ya nchi pamoja na shughuli nyingine za chama tawala wa cha wafanyakazi.

Hata ni mara chache bunge hili hutoa maamuzi magumu, mfano mwaka 2012 liliidhinisha na mabadiliko kwenye katiba na kuitangaza nchi hiyo kama nchi ya nyuklia.

Taarifa iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa KCNA imesema kuwa mkutano mkuu wa bunge la jamhuri ya Korea Kaskazini litaketi April 11.

hata hivyo taarifa hiyo haikuweka wazi masuala ambayo huenda yatajadiliwa katika kikao hicho.

Mhadhiri wa taasisi ya Sejong, Cheong Seong-Chang amesema kuwa kikao cha bunge hili huenda kikashuhudia kufanyika kwa mabadiliko ya viongozi wa juu ili kurahisha mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo na jumuiya ya kimataifa.

Moja ya viongozi wanaotajwa kuwa huenda wakang'oka kwenye nafasi zao ni Kim Yong Nam ambaye alifanya ziara ya kikazi wakati wa michezo ya Olimpiki nchini Korea Kusini, alisema Cheong.

Nafasi ya Nam mwenye umri wa miaka 90 huenda ikachukuliwa na waziri wa sasa wa mambo ya kigeni Ri Yong Ho ambaye ametoa mchango mkubwa katika juhudi zainzoshuhudiwa hivi sasa za mazungumzo kati ya nchi hiyo na Korea Kusini pamoja na Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.