Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI

Viongozi wa Korea Kusini na Kaskazini kukutana April 27

Waziri wa muungano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon (kushoto) akiwa na mwenzake wa Korea Kaskazini Ri Son Gwon (kulia). 29 Machi 2018.
Waziri wa muungano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon (kushoto) akiwa na mwenzake wa Korea Kaskazini Ri Son Gwon (kulia). 29 Machi 2018. Korea Pool/Yonhap via REUTERS

Nchi za Korea zimekubaliana tarehe ya mkutano baina ya nchi hizo mbili, mkutano unaotokana na mazungumzo ya hivi karibuni kati ya ujumbe wa Korea Kusini uliosafiri kuonana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un.

Matangazo ya kibiashara

“Kutokana na utayari wa viongozi wa pande zote mbili, wamekubaliana kufanya mkutano wa South-North tarehe 27 ya mwezi April 2018 katika ofisi zinazotumiwa na pande hizo mbili kwenye mji wa Panmunjom,” imesema taarifa yao ya pamoja.

Mkutano kati ya Kim Jong-Un kiongozi wa Korea Kaskazini na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in utakuwa ni watatu wa aina hiyo na utafuatiwa na mkutano wa aina yake kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Kim Jong-un, mapema mwezi Mei.

Mahali pa mkutano huu kutamfanya Kim Jong Un kukanyaga ardhi ya Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, licha ya kuwa babu yake Kim Il Sung kuwahi kutembelea eneo hilo mara kadhaa.

Pande hizo mbili pia hazijakubaliana nini kinapaswa kuwa kwenye ajenda ya mazungumzo yao, lakini kiongozi wa ujumbe wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon amewaambia waandishi wa habari kuwa wamekubaliana Kim na Moon kuwa na mazungumzo ya wazi.

Mazungumzo hayo yatahusu pia kuhusu nchi hiyo kuachana na mpango wake wa nyuklia, alisema Cho.

Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Pyongyang Ri Son Gwon aliongeza kuwa “Kile watu wanachotaka ni ajenda yetu.”

Mkutano mwingine utafanyika Jumatano ya wiki ijayo kati ya ujumbe wa pande hizo mbili kuzungumzia masuala ya kiitifaki na usalama kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi.

Mkutano wa mwezi ujao unakuja baada ya mikutano mingine kama hiyo mjini Pyongyang mwaka 2000 na 2007 ambapo tangu wakati huo Korea Kaskazini ilipiga hatua katika kutengeneza silaha za maangamizi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.