Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Korea kaskazini yasitisha mkutano wake na Korea Kusini

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wako tayari kuleta amani katika rasi ya Korea.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in (kulia) na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wako tayari kuleta amani katika rasi ya Korea. REUTERS

Korea Kaskazini imefuta ghafla mkutano wake na Korea Kusini uliokuwa unatarajiwa kufanyika Jumatano Mei 16 kufuatia mazoezi ya kijeshi kwa ushirikiano na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limesema kwamba mazoezi hayo ya kijeshi ni "uchokozi" na maandalizi ya uvamizi, jambo linaloashiria kurejelewa kwa lugha kali iliyokuwa inatumiwa wakati wa uhasama kati ya Marekani na Korea Kusini.

“Korea Kaskazini imesitisha mazungumzo yaliyotarajiwa kufanyika mapema wiki hii dhidi ya Korea ya Kusini kwa sababu ya kuchukizwa kwake na mazoezi ya kijeshi ya pamoja na Marekani, “ amesema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Kim Kye-gwan.

Maafisa wa ngazi ya juu wa mataifa hayo walitarajiwa kukutana katika eneo la mpakani ambapo majeshi hayaruhusiwi kujadiliana maelezo zaidi kuhusu makubaliano ambayo yalikuwa yameafikiwa katika mkutano mkuu kati ya mataifa hayo mwezi uliopita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.