Pata taarifa kuu
ARMENIA-FRANCOPHONIE-USHIRIKIANO

Mkutano wa Francophonie waendelea Erevan

Mkutano wa 17 wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophonie, (OIF), Erevan, Armenia.
Mkutano wa 17 wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophonie, (OIF), Erevan, Armenia. Ludovic MARIN / AFP

Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa (Francophonie) unaendelea Ijuma wiki hii huko Erevan nchini Armenia.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wanatarajiwa kumteuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kuwa katibu mkuu wa Jumuiya hiyo, kuchukuwa nafasi ya Michaelle Jean.

Katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo, nchi wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Francophonie (OIF) watamchaguwa katibu mkuu mpya kati ya Louise Mushikiwabo na Michaëlle Jean kutoka Canada.

Michaelle Jean, mwanasiasa wa zamani na mwandishi wa habari mwenye asili ya Canada, alijikuta uungwaji wake mkono wa kuchaguliwa ukipungua hata kabla ya kuanza kwa mkutano huo, baada ya Canada na Quebec kutangaza kutomuunga mkono.

Katibu mkuu wa sasa Michaelle Jean ambae hata hivyo uongozi wake hauangaliwi kwa mtazamo chanya na nchi zote wanachama amesema Juimuiya hiyo imepiga hatua licha mitikisiko ya kisiasa katika baadhi ya nchi wanachama.

Akizungumza katika mkutano huo, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amejigamba kujivunia Jumuiya hiyo, ambayo amesema hakuna nchi inayotoa amri dhidi ya nyingine.

Inaelezwa kuwa kawaida viongozi wa Jumuiya hiyo ya nchi 84 kutoka katika dunia kote, huafikiana kuhusu uteuzi wa katibu mkuu, lakini aliepo sasa Michaelle Jean amekataa kuachia nafasi na kumpisha Louise Mushikiwabo, akitaka upigaji kura.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.