Pata taarifa kuu
INDONESIA-AJALI

Indonesia: Kisanduku cha pili cheusi cha ndege ya Lion Air chapatikana

Ndege za mashirika ya ndege ya Indonesia zaendelea kukumbwa na ajali.
Ndege za mashirika ya ndege ya Indonesia zaendelea kukumbwa na ajali. REUTERS/Beawiharta

Kikosi cha Indonesia kilichokuwa kikitafuta mabaki ya ndege ya Boeing 737 MAX ya shirika la ndege ya Lion Air iliyoanguka Oktoba 29 katika Bahari ya Java, na kuua watu 189, kinasema kimepata kisanduku cha pili cheusi cha kuhifadhi mawasiliano ya ndege.

Matangazo ya kibiashara

Luteni Kanali Agung Nugroho ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa ishara ya kiwango cha chini kutoka chombo cha kuhifadhi mawasiliano iligunduliwa kwa siku kadhaa na kwamba kisanduku cheusi kimepatikana kutoka chini ya mita telathini ya urefu wa kina.

Kisanduku ca kwanza cheusi ikilipatikana bila kasoro yoyote chini ya bahari mnamo mwezi Novemba mwaka jana.

Wachunguzi wanajaribu kubaini kwa nini rubani aliomba kurejea nyuma kabla ya kupoteza mawasiliano, baada ya dakika 13 ndege hiyo ikipaa hewani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.