Pata taarifa kuu
CHINA-USALAMA

China yaagiza kusitishwa kwa safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX

Mamlaka ya usafiri wa anga ya China (CAAC) imesema katika taarifa yake kwamba itajulisha mashirika ya ndege uwezekano wa safari za ndege hizo kuanza tena, baada ya kuwasiliana na kampuni ya Boeing na mamlaka nchini Marekani.
Mamlaka ya usafiri wa anga ya China (CAAC) imesema katika taarifa yake kwamba itajulisha mashirika ya ndege uwezekano wa safari za ndege hizo kuanza tena, baada ya kuwasiliana na kampuni ya Boeing na mamlaka nchini Marekani. © REUTERS

Mamlaka nchini China imeagiza mashirika ya ndege nchini humo kusitisha safari za ndege zao aina ya Boeing 737 MAX, baada ya ajali mbaya ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines kuua watu 157 jijini Addis Ababa, Jumapili Asubuhi MAchi 10, 2019.

Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea mapema Jumapili asubuhi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa.

Raia tisa wa Ufaransa ni miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Mnamo mwezi Oktoba, ndege nyingine aina ya Boeing 737 MAX 8, ya shirika la ndege la Simba Air, alianguka katika Bahari ya Java, na kuua watu 189. Sababu ya ajali hiyo, iliyotokea muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, hazikuelezwa.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya China (CAAC) imesema katika taarifa yake kwamba itajulisha mashirika ya ndege uwezekano wa safari za ndege hizo kuanza tena, baada ya kuwasiliana na kampuni ya Boeing na mamlaka nchini Marekani.

"Kwa kuwa ajali zote mbili zinahusisha ndege za Boeing 737-8 zilizonunuliwa hivi karibuni na ni ajali ambazo zilitokea wakati wa kuruka, kuna baadhi ya mambo yanayofanana," CAAC imesema, ikiongeza kuwa uamuzi huu unaendana na kanuni za usalama.

Mashirika ya ndege ya China yana ndege 96 aina ya Boeing 737 MAX, mamlaka imesema.

Gazeti la Caijing linaripoti kwamba safari nyingi za ndege zilizopangwa kutumiwa na ndege hizo hutumiwa na ndege aina ya Boeing 737-800.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.