Pata taarifa kuu

Brunei: Muungano wa kimataifa walaani adhabu ya kifo dhidi ya mashoga

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Brune, Begawan Aprili 22, 2013.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Brune, Begawan Aprili 22, 2013. REUTERS/Bazuki Muhammad

Nchi zaidi ya 30, ambazo zinaongozwa na Canada, zimeomba Brunei kufuta adhabu ya kifo iliyopitishwa hivi karibuni dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na adhabu nyingine kali.

Matangazo ya kibiashara

Muungano kwa Haki sawa (CDE) ulielezea katika taarifa ya mwishoni mwa wiki hii iliyopita "masikitiko yake makubwa" baada ya uongozi wa nchi hiyo kupitisha "adhabu kali" chini ya sheria mpya ya jinai kulingana na sheria za dini (Sharia).

"Tunahimiza serikali ya Brunei kufuta hukumu mpya na kuhakikisha kwamba hatua yoyote iliyopitishwa inaendana na sheria za kimataifa za haki za binadamu," taarifa hiyo imebaini.

Adhabu mpya zina "matokeo mabaya kwa makundi mengi ya wanyonge nchini Brunei, ikiwa ni pamoja na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, wanawake na watoto" na "huongeza hatari ya ubaguzi, mateso na vurugu, "inasema taarifa iliyosainiwa na nchi 36.

Mbali na kupigwa mawe kwa watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja au uzinzi, sheria hiyo mpya ya jinai ya Brunei pia inaruhusu kukatwa mkono au mguu mwizi. Hatia ya kubaka au kumkashifu Mtume Muhammad inaadhibiwa na kifo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.