Pata taarifa kuu
SRI LANKA-USALAMA-UCHUNGUZI

Sri Lanka: Mkuu wa Polisi ajiuzulu kufuatia mashambulizi

Siri Lanka Ijumaa 26 Aprili, askari wakitoa ulinzi nje ya Msikiti Mkuu (Grand Mosque)  Negombo.
Siri Lanka Ijumaa 26 Aprili, askari wakitoa ulinzi nje ya Msikiti Mkuu (Grand Mosque) Negombo. ATHIT PERAWONGMETHA

Mkuu wa polisi wa Sri Lanka amejiuzulu baada ya mashambulizi ya Jumapili ya Pasaka ambayo yaligharimu maisha ya watu 253 katika kisiwa cha Asia Kusini, rais Maithripala Sirisena ametangaza leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

"Mkuu wa Polisi amejiuzulu," amesema rais Sirisena wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Pujith Jayasundara ni afisa mwandamizi wa pili wa Sri Lanka kuachia ngazi kutokana na kushindwa kwa mamlaka kuzuia mauaji baada ya afisa wa ngazi juu kwenye wizara ya ulinzi kujiuzulu Alhamisi jioni.

Serikali ya Sri Lanka imekiri kuwa, kulikuwa na kuupuzwa kwa taarifa za kiiteljensia kabla ya shambulizi la bomu wakati wa sikukuu ya Pasaka, lililosababisha vifo vya watu 359 na kusababisha watu wengine 500 kujeruhiwa.

Ripoti zinasema kuwa, Inteljensia kutoka nchini India, zilieleza kuwa kulikuwa na uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya bomu yakilenga makanisa na hoteli, na taarifa hiyo iliwafikia wakuu wa usalama nchini humo.

Washambuliaji nane kati ya tisa wanaoaminiwa walihusika, wote ni rais wa Sri Lanka, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka Sri Lanka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.