Pata taarifa kuu
JAPANI-CHINA-USHIRIKIANO

Mkataba wa kugawana taarifa za kijeshi wavunjika: Tokyo yapinga vikali uamuzi wa Seoul

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Taro Kono Akizungumza mjini Bangkok, Agosti 2, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Taro Kono Akizungumza mjini Bangkok, Agosti 2, 2019 © AFP

Tokyo "imepinga vikali" uamuzi wa Korea Kusini wa kuvunja mkataba wa kugawana taarifa za kiintelijensia, waziri wa mambo ya nje wa Japani amesema leo Alhamisi, na kudai kuwa hatua hiyo "inasikitisha sana."

Matangazo ya kibiashara

"Napaswa kusema kwamba uamuzi wa kusitisha mkataba huu uliochukuliwa na serikali ya Korea Kusini ni makosa kabisa kuhusu hali ya usalama wa kanda hii na inasikitisha sana," Taro Kono amesema katika taarifa.

"Hatuwezi kukubali madai ya Korea Kusini na tutapinga vikali uamuzi huo mbele ya Serikali ya Korea Kusini," Kono ameongeza.

Awali Serikali ya Seoul ilitangaza kwamba "haikuwa kwa maslahi ya kitaifa kuendelea na mkataba uliyolitiliwa saini kwa lengo la kubadilishana taarifa muhimu za kiintelijensia".

Uhusiano kati ya Tokyo na Seoul umeingiliwa na dosari kwa miongo kadhaa kutokana na tofauti za zamani kutoka wakati ambapo kanda hiyo ilikuwa koloni la Japan (1910-1945).

Na mzozo huu wa kimya kimya unaihangaisha Washington, ambayo inategemea ushirikiano kati ya Japani na Korea Kusini ili kuunga mkono sera yake katika eneo lenye utata mkubwa kutokana na tishio la nyuklia la Korea Kaskazini na China kuendelea kimaendelea katika zana zake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.