Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Hong Kong: Mwanaharakati anayetetea demokrasia Joshua Wong akamatwa

Joshua Wong katika maandamano Juni 17, 2019, Hong Kong.
Joshua Wong katika maandamano Juni 17, 2019, Hong Kong. REUTERS/Thomas Peter

Mwanaharakati anayetetea demokrasia Hong Kong, Joshua Wong, amekamatwa leo Ijumaa (Agosti 30) siku moja kabla ya maandamano mapya yanayoendelea katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa Hong Kong, wanaharakjati wengine Agnès Chow, kutoka chama kimoja na Joshua Wong, na Andy Chan, pia wamekamatwa.

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha Demosisto, Nathan Law, Joshua Wong alingizwa katika gari lisilo kuwa nambari za usajili saa 7:30 asubuhi alipokuwa akitoka nyumbani kwake akielekea kituo cha treni ya mwendo kasi cha South Horizon katika kitongoji chake, kinachopatikana kwenye kisiwa cha Ap Lei Chau.

Amepelekwa katika kituo kikuu cha Polisi cha Wan Chai. Polisi imethibitisha kumkamata mwanaharakati huyo. Joshua Wong aliachiliwa kutoka jela mnamo Juni 17 wakati alikuwa amemaliza kutumikia kifungo cha miezi michache kwa machafuko yanayohusiana na "vuguvugu la watu waliokuwa wakiandamana wakitumia miamvuli kujikinga na moshi wa mabomu ya machozi" miaka mitano iliyopita.

Saa chache baadaye, polisi imetangaza kumkamata Agnes Chow, mmoja kati ya viongozi wa chama cha Demosisto.

Kiongozi mwingine mwanafunzi, Andy Chan, mwanzilishi wa chama cha HKNP, ambacho kwa sasa kimepigwa marufuku, amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wakati alikuwa akisafiri kwenda Japan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.