Pata taarifa kuu
CHINA-SIASA-UCHUMI-USALAMA

China yaadhimisha miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China

Gwaride la kijeshi kwenye eneo la Tiananmen, Beijing, Oktoba 1, 2019.
Gwaride la kijeshi kwenye eneo la Tiananmen, Beijing, Oktoba 1, 2019. Greg BAKER / AFP

Sherehe ya maadhinisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China kuanzishwa imeanza tangu mapema asubuhi Jumanne hii Oktoba Mosi kwenye Uwanja wa Tian'anmen, katikati ya mji wa Beijing.

Matangazo ya kibiashara

Gwaride la kijeshi na gwaride la umma zitafanyika baada ya Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye pia ni rais wa China na katibu mkuu wa kamati kuu ya Kijeshi Xi Jinping kutoa hotuba.

Vituo vya redio, televisheni na matovuti ya habari vitatangaza moja kwa moja sherehe hizo, gwaride na maonyesho ya umma.

Habari zinasema, Jumanne hii jioni, maonyesho mbalimbali ya kusherehekea siku ya taifa la China yatafanyika kwenye Uwanja wa Tian'anmen.

China ni nchi kubwa ya Asia ya Mashariki ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote duniani.

China imepakana na Vietnam, Laos, Myanmar, India, Bhutan, Nepal, Pakistan, Afghanistan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Kazakhstan, Urusi, Mongolia, Korea ya Kaskazini.

China kuna makabila 56 tofauti. Wahan ndio kabila kubwa zaidi nchini China kwa idadi ya watu ikiwa na asilimia 92.

Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin kinachotumiwa na asilimia 70 za wananchi.

Siasa inatawaliwa na chama cha kikomunisti.

Mji mkuu ni Beijing lakini Shanghai ndio mji mkubwa zaidi.

Hong Kong iliyokuwa koloni la Uingereza na Macau iliyokuwa koloni la Ureno ni maeneo ya China yenye utawala wa pekee.

Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazamwa na serikali ya Beijing kuwa majimbo yake lakini vimekuwa kama nchi ya pekee tangu mwaka 1949.

Jiografia

China ina eneo la kilomita za mraba milioni 9.6 hivyo ni nchi ya tatu au ya nne[1] kwa ukubwa duniani.

Sura ya nchi inaonyesha tabia tofautitofauti.

Upande wa kaskazini, mpakani mwa Siberia na Mongolia, kuna maeneo yabisi pamoja na jangwa la Gobi.

Kinyume chake upande wa kusini, mpakani mwa Vietnam, Laos na Burma, hali ya hewa ni nusutropiki yenye mvua nyingi inayolisha misitu minene.

Sehemu za magharibi zina milima mingi ambayo ni kati ya milima mirefu duniani kama Himalaya na Tian Shan.

Mashariki ya nchi huwa na tambarare zenye rutuba na hapa ndipo kanda lenye wakazi wengi.

Upana wa China kati ya kaskazini na kusini ni kilomita 4,200 na kati ya mashariki na magharibi ni kilomita 4,200.

Pwani ina urefu wa kilomita 14,400.

Kuna mito mikubwa; mrefu zaidi ni Yangtse (km 6,300), Hwangho au Mto Njano, Xi Jiang au mto wa Magharibi, Mekong, Mto wa Lulu, Brahmaputra na Amur. Mito hiyo yote ina vyanzo vyake katika milima mikubwa yenye usimbishaji mwingi, ikibeba maji kwenda tambarare pasipo mvua nyingi.

Jiografia hiyo ilikuwa chanzo cha kilimo cha umwagiliaji na kukua kwa madola ya kwanza.

Kutokana na madawa ya kilimo na maji machafu ya viwanda, mito na maziwa ya China hupambana na machafuko makali; mwaka 2007 ziwa Tai lilisafishwa kwa gharama kubwa mno kwa sababu maji hayakufaa tena kwa mahitaji ya binadamu (maji ya bomba).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.