Pata taarifa kuu
JAPAN-KIMBUNGA-USALAMA

Kimbunga Hagibis: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 70 Japan (NHK)

Mvua kubwa na kimbunga Hagibis vimesababisha na hasara kubwa katika eneo la Setagaya jijini Tokyo.
Mvua kubwa na kimbunga Hagibis vimesababisha na hasara kubwa katika eneo la Setagaya jijini Tokyo. Reuters

Kimbunga Hagibis, ambacho kilipiga maeneo kadhaa ya Japan kati ya Jumamosi na Jumapili, kimeuwa watu karibu 70, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Jumanne na kituo cha televisheni cha umma NHK.

Matangazo ya kibiashara

Watu kumi na tano hawajulikani waliko, NHK imeripoti.

Zaidi ya waokoaji 100,000 wanaendelea kutafuta manusura katika maeneo yaliyojaa mafuriko na ambayo yameathiriwa na maporomoko mabaya ya udongo, yaliyosababishwa na mvua "ambazo hazijawahi kutokea" zilizoambatana na kimbunga Hagibis, kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa wa Japani.

Idadi hiyo iliendelea kuongezeka hadi Jumatatu wiki hii, kulingana na ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa kulinagna na habari zilizokusanywa kutoka maeneo mbalimbali na waandishi wa habari wa kituo hicho cha televisheni ya serikali. NHK imetoa jumla ya idadi ya watu 70 Jumanne hii, ambao wamepoteza maisha kufuatia kimbunga hicho.

Hata hivyo maeneo kadhaa bado yanakabiliwa na kitisho cha kutokea zitakazosababishwa na kimbunga hicho pamoja na mvua. Wadadisi wanasema askari, maafisa wa zima moto, polisi na walinzi wa pwani watakuwa na kazi ngumu ya kukabiliana na hali hiyo hasa kwa kuokoa maisha ya wakaazi wa maeneo hayo ambayo yako katika hatari ya kukumbwa na kimbunga Hagibis.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.